Kituo
cha polisi kilichopo ushirombo wilayani Bukombe mkoani
Geita kimevamiwa na majambazi usiku wa saa tisa kuamkia
leo huku askari wawili wakiuawa na watatu wakijeruhiwa vibaya
Ambapo
taarifa za awali zinasema kuwa licha ya matukio
hayo wamelipua chumba cha kuwekea silaha na zingine kuondoka nazo,pia
wamefanikiwa kuondoka na bunduki zaidi ya 5 aina ya SMG na kutokomea
nazo
Watu
wamekusanyika kituoni hapo kushuhudia huku kituo hicho kikiwa
kimezungushiwa kamba nyekundu kwa kusitisha huduma na
mahabusu waliokuwemo wamehamishwa.
Hata hivyo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Geita Joseph Konyo yupo katika eneo la tukio kwa uchunguzi zaidi .
credit ..malunde.blog