Kesi
ya aliyejifanya askari polisi wa usalama barabarani, James Hassan (45)
imeendelea kupigwa kalenda kutokana na mshitakiwa kutofika mahakamani
hapo licha ya kuwepo kwa mashahidi wawili.
Kesi
hiyo iliyofikia hatua ya kusikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya
Ilala, imekuwa ikipigwa kalenda mara kwa mara kutokana na mshitakiwa
huyo kudai kwamba anaumwa hivyo kukwamisha kesi hiyo kuendelea.
Wakili
wa Serikali, Felista Mosha alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,
Hassan Juma kwamba mashahidi wawili wamefika mahakamani hapo kwa ajili
ya kutoa ushahidi wao lakini kutokana na mshitakiwa kuwa mgonjwa,
aliomba tarehe nyingine ya kusikiliza shauri hilo.
Hakimu Juma alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha shauri hilo hadi Septemba 24, mwaka huu kwa hatua za usikilizwaji.
Shahidi
wa pili katika kesi hiyo aliieleza Mahakama jinsi mshitakiwa
alivyojipatia sare za askari polisi kutoka kwa marehemu baba yake mdogo
na kujifanya askari wa usalama barabarani.
Mshitakiwa
huyo alifikishwa mahakamani Agosti 14, mwaka jana, kujibu mashitaka ya
kujifanya askari polisi baada ya kukutwa Kinyerezi Mnara wa Voda na
kukana mashitaka hayo. Yupo rumande.
0 Comments