Na Mwandishi wetu
Mbunge
wa Kawe Halima Mdee CHADEMA amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la
wanawake wa Chama hicho (BAVICHA) unaoendelea katika ukumbi wa Mlimani
City.
Akizungumza
baada ya uchaguzi huo, Mdee aliwaasa wanawake kwa wanawake kuwa wamoja
badala ya kupigana vijembe wao kwa wao ili maendeleo ya mwanamke yaweze
kupatina na na kuondokana na mfumo dume
“Nimezoea
kuona watu wanaotukashifu ni wa upande wa pili kutokana na mfumo dume
uliojengeka na sio wanawake wenyewe kukashifiana,” alisema.
Alisema
mwanamke ana nguvu ya kuleta mabadiliko na kueleza kuwa, Chama Cha
Mapinduzi (CCM), kipo madarakani kwa sababu kinawatumia wanawake na
kutaka nao kuungana na kuwa kitu kimoja.
“Mwanamke
ana nguvu ya kuleta mabadiliko, bila kuwatumia hakuna ushindi na
wanawake siku zote wanamsimamo na sio wasaliti hata kidogo,” alisema
Mdee.
Aidha aliwataka wanawake wakafanye kazi majimboni kwa umoja licha ya kufahamu wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa fedha.
“Harakati
zetu sio za starehe na hata ikiwezekana pindi mnapokuwa majimboni bila
kujali mnalala wapi, mnatumia choo cha ‘pasipoti size’ ili mradi ushindi
unapatikana,” alisema.
Akitangaza
matokeo hayo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana,
Arcado Ntagazwa, alisema Mdee alipata kura 165 akifuatiwa na Janeth
Rithe 35, Sophia Mwakagenda 18, Chiku Abwao 15, Lilian Wassira 11 na
Rebecca Magwishe kura 4.
Kwa
upande wa Makamu Mwenyekiti upande wa Bara, alitangazwa Hawa Mwaifunga
aliyejinyakulia kura 136 akifuatiwa na Victoria Benedict kura 99.
Nafasi
ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar ilichukuliwa na Hamida Abdalah Huewishi
aliyepata kura 194 akifuatiwa na Mariamu Msabaha kura 36.
0 Comments