Mfungwa mmoja nchini Kenya
amewaacha wengi vinywa wazi, baada ya simu tatu za mkononi kutolewa
mwilini mwake. Inaarifia aliziingiza simu hizo mwilini mwake kupitia
sehemu yake nyeti ya nyuma.
Mfungwa huyo wa gereza la King’ong’o
katika jimbo la Nyeri alifanyiwa upasuaji Jumanne kutolewa simu hizo
ambazo alikuwa amezificha mwilini mwake kupitia sehemu yake ya nyuma.
Mfungwa ambaye alitolewa simu mwilini kwa kufanyiwa upasuaji
Tatizo la kuingiza bidhaa kimagendo ndani ya magereza ni kero kubwa kwa maafisa wakuu wa magereza.
Wamekuwa kwa miaka mingi
wakijaribu kulikomesha tatizo hilo bila mafanikio.Kwa njia yoyote ile
wafungwa huingiza bidhaa kama simu katika magereza nchini Kenya kinyume
na sheria za magereza.
Maafisa wa magereza wanakiri kwamba
wafungwa hawa wakati mwingine hushirikiana na walinzi wa magereza
kuingiza bidhaa katika magereza kimagendo.
0 Comments