Mwalimu
mmoja nchini Kenya, ambaye aliibiwa fedha zake na yeye mwenyewe
kupigiliwa msumari kwenye mti, amezungumzia mkasa huo. Wezi hao
walimuibia dola ishirini na nne Peter Asutsa Alhamisi iliyopita, kabla
ya kuupigilia kwa msumari mkono wake kwenye mti katika msitu mmoja
uliopo Eldoret, magharibi mwa Kenya. Mwalimu huyo wa mafunzo ya Jumapili
(Sunday School) alikaa kwa saa kumi na sita akiwa katika maumivu makali
kabla ya kuokolewa na polisi. Amesema aliweza kuwasiliana na mke wake
kwa kutumia simu yake aliyokuwa ameificha kwenye nguo yake ya ndani.
(Picha: | JARED NYATAYA | NATION MEDIA GROUP)