JESHI la Polisi linawashikilia wafanyakazi wa Kiwanda cha Mtava
kutokana na kudaiwa kula njama na kuhusika na uporaji wa sh milioni 5.9
uliotokea katika barabara ya Shaurimoyo na Nyerere jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza nasi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kipolisi Ilala, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Mary Nzuki,
alisema wafanyakazi hao wanashikiliwa kutokana na tukio la uporaji
lilitokokea katika barabara ya Shaurimoyo juzi saa 10 jioni.
Kamanda Nzuki, alisema kuwa Tutu Mtabalezi (32), na Cletus Mathew
‘Lilungulu’ (46), wakiwa katika gari namba T875 AZU Toyota Mark II
maeneo ya Shaurimoyo, walivamiwa na mtu mmoja aliyekuwa katika pikipiki
aina ya Boxer na kufanikiwa kupora kiasi hicho cha fedha na kutokomea
kusikojulikana.
“Mathew ambaye ni Meneja Utawala na Mtabalezi Meneja Msaidizi walikuwa
wakitokea kuchukua fedha za mauzo za kampuni hiyo maeneo ya Msimbazi,
ndipo walipofika Shaurimoyo katika foleni wakavamiwa na watu hao
waliokuwa katika pikipiki na kuporwa,” alisema.
Alisema kuwa, hadi sasa Jeshi la Polisi linaendelea kuchunguza tukio hilo huku likiwashikilia wafanyakazi hao.
0 Comments