Kufuatia
ajali mbaya ya ajali huko wilayani Butiama mkoani Mara,iliyoua watu
36,majeruhi 79,Serengeti Fiesta 2014 Shinyanga ilipaswa kufanyika leo
Septemba 7,2014 katika uwanja wa CCM Kambarage imeahirishwa mpaka hapo
baada taarifa nyingine itakapotolewa. Lakini lile shindano la kumsaka
Serengeti SUPA NYOTA DIVA litafanyika kama kawaida katika ukumbi wa RAY
MISANGA CCM WILAYA mjini Shinyanga kuanzia saa 3 asubuhi kesho Jumapili
Septemba 7,2014. Jana Serengeti Fiesta Musoma pia iliahirishwa kutokana na sababu ya ajali hiyo mbaya |