Shuhuda aliyenusurika
kwenye mauaji ya Albino ambaye amekatwa mikono yote miwili, Mariam
Stanford akitoa ushuhuda wake na killio chake mbele ya meza na wageni
waalikwa waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya
amani iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya
Mnazi mmoja.
Na Mwandishi wetu
Mwanamke
albino Mariam Stanford aliyepoteza mikono yake yote miwili wakati
iliponyofolewa na majahili asiowajua Oktona7, 2008 ameitaka serikali
kuwanyonga wote wanaopatikana na hatia ya kuua albino nchini.
Alisema hata adhabu ya
kifungo cha maisha haiwatoshi kwa jinsi wanavyosababisha maisha ya
mashaka na yenye uchungu kwa walemavu wa ngozi.
Akiongea kwa uchungu
huku hapa na pale akitulia kwa kuzidiwa na machozi kiasi cha kushidwa
kuzungumza Stanford ambaye alisema wakati akikatwa mikono yake alikuwa
na mimba ya miezi mitano na ambayo ilitoka alisema majahili hao si wa
kusamehewa.
Alisema akiwa mama wa
familia kitendo cha kumuondolea mikono yake kimemfanya kuwa tegemezi
hali ambayo inaongeza maumivu juu ya maumivu ambayo anayo ya
kunyanyapaliwa na jamii.
Alisema hayo wakati
akitoa ushuhuda katika adhimisho la siku ya amani duniani iliyofanyika
kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Alisema japokuwa
Tanzania inaelezwa kuwa nchi ya amani wananchi wake wenye ulemavu wa
albino hawana amani kutokana na kuwindwa kama digidigi. Alisema kwa sasa
Tanzania ni kisiwa cha matatzio kwa kundi hilo ambalo sasa linajificha
na wala kutokujua kesho ikoje au siku hiyo ikoje.
Mke wa Balozi wa
Uturuki nchini Yesim Davutoglu, akilia kwa uchungu baada ya kusikia
shuhuda kutoka kwa mhanga wa mauaji ya Albino aliyekatwa mikono yote
miwili, Mariam Stanford (hayupo pichani) ambaye hadi sasa anapewa
matunzo na Shirika la Under The Same Sun.
Alisema ni vyema jamii
ikawatazama na kuwasaidia kwa kuhakikisha kwamba wanasaidia kuwafichua
watenda maovu hao hasa ikizingatiwa kwamba watu wenye albinizimu ni watu
na watu kama watu wengine na hawawezi kuwa chanzo cha utajiri kwa
binadamu wenzao.
Alisema anatamani kuona
waliotiwa hatiani wakiuuawa hadharani au hata watu hao nao kukatwa
viungo vyao ili watambue jinsi isivyofaa kuwafanyia binadamu wenzao
matendo hayo.
Alishukuru taasisi ya
Under the Same Sun kwa kumsaidia toka aliponyofolewa mikono mpaka leo na
kuhimiza serikali kuona namna ya kuwasaidia waliokatwa viungo vyao ili
waweze kusihi maisha ya kawaida.
Mkurugenzi Mtendaji
wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akimfariji mke wa Balozi
wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, wakati wa maadhimisho ya siku ya
kimataifa ya amani duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja
hivi karibuni jijini Dar.
Pamoja na kuomba watu
hao wanyongwe Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali George Masaju aliitaka
jamii kutambua kwamba sheria ya kuua anayeua ipo lakini inakabiliwa na
mashindano na wanaharakati huku watoa ushahidi wakishindwa kuisaidia
mahakama kufikia maamuzi katika kesi za maalbino.
Alisema ni wajibu wa wananchi kusimamia amani kwa kuhakikisha wanaisaidia serikali kutekeleza wajibu wake.
Balozi wa Uturuki
nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu akisoma ujumbe kwa niaba wa umoja wa
mabalozi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani.
Naye Balozi wa Uturuki
nchini alisema kwamba Ali Davutoglu amesema kwamba ujenzi wa kituo cha
maalbino Bagamoyo utaanza hivi karibuni ili kuwapatia nafasi wananchi
hao kuwa katika hali ya kawaida.
Kituo hicho ambacho kitakuwa na uwezo wa kuchukua watu 500 na kuwa chemchem ya maarifa kwa watu wenye albinizimu.
Katika adhimisho hilo
watoto wenye albuinizim walitoa shoo ya nguvu iliyowafanya watu
mbalimbali kujimwayamwaya katika eneo la wazi na kutoa zawadi kwa vijana
hao.
Aidha bendi ya vijana
ilitumbuiza na kwaya ilikuwepo kutoa ushaiwishi wa kuelewa umuhimu wa
amani huku wazungumzaji wengine wakitaka wanasiasa kuhudhura maadhimisho
hayo na kupeleka ujumbe kwa wananchi ambao wanawasikiliza.
Katika adhimisho hilo
wanasiasa waliokuwepo ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa dar es salaam,
Madabida, Kaimu katibu Mkuu NCCR-Mageuzi Faustin Sungura na Naibu
katibu mkuu CUF Magdalena Hamis Sakaya ambaye pia ni mbunge wa viti
maalumu Tabora.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali, George Masaju, akizungumza kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar.
Mgeni rasmi kwenye
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii, Mh. Seif Rashid (wa pili kushoto), Mratibu Mkazi wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia), Makamu Mwenyekiti wa
Chama cha Albino Tanzania (TAS), Joseph Masasi, kwenye picha ya pamoja
na binti mhanga wa mauaji ya Albino aliyekatwa mikono yote miwili,
Mariam Stanford (kushoto).
0 Comments