Mwili
wa marehemu Musa Shija mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa mtaa wa
Mwalugoye kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga aliyeuawa kwa
kushambuliwa akiwa kwenye Fiesta usiku wa kuamkia leo katika uwanja
mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga ukiwa katika chumba cha kuhifadhia
maiti katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza na Malunde1 blog mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa amesema uchunguzi wa kitaalam walioufanya unaonesha kuwa kijana huyo alipigwa na kitu butu kichwani na kusababisha kuvuja damu kichwani kutokana na kuvunjika kwa fuvu la kichwa.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga
Mussa Athuman amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi wa awali
unaonesha kuwa kijana huyo aliuawa kwa kushambuliwa na watu wasiojulikana nje
ya fensi la uwanja mdogo wa Kambarage palipokuwa panafanyika tamasha la Fiesta.
Hata
hivyo amesema jeshi la polisi litatoa taarifa kamili baadaye kwani
linaendelea kufanya uchunguzi ili kujua chanzo cha tukio
Na Kadama Malunde-Shinyanga
0 Comments