Aliekuwemo kwenye hili basi ndio amenitumia hizi picha na kuniambia watu wasiozidi watano wamefariki dunia wengine zaidi kujeruhiwa baada ya basi lao kuanguka Mkange Berega.
Basi linaitwa Air Bus
na limepata ajali likielekea Dodoma kutokea Morogo na ni baada ya kifaa
cha usukani kushindwa kufanya kazi ambapo muda mfupi baadae anasema
alisikia tu dereva akipiga kelele na kisha kikafata kishindo, basi
likaacha njia na kwenda bondeni.
millardayo.com inaendelea
kufatilia ili kupata taarifa kamili ili kujua idadi ya vifo na majeruhi
pamoja na taarifa nyingine ambapo ajali hii imetokea siku tatu baada ya
Waziri wa uchukuzi Dr. Harryson Mwakyembe kufungia kampuni mbili za
mabasi ya J4 Express na Mwanza Coach yaliyogongana na kuua 39 Musoma.