JESHI la
polisi mkoa Kigoma limefanikiwa kukamata silaha za kivita aina ya SMG, mabomu
matatu ya kutupa kwa mkono, risasi 64 pamoja na kuwauwa watu watano
wanaosadiliwa kuwa ni majambazi wakati wa purukushani za majibizano baina
majambazi hao na askari polisi mkoani Kigoma.
Akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari mkoani humo kamishina msaidizi wa polisi mkoa
kamanda Japhal Ibrahim alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 11:45
alfajiri Septemba 3 mwaka huu, katika barabara kuu ya Kasulu – Kibondo eneo la
pori la Malagalasi Wilayani Kasulu.
|