Mama anayedaiwa kumsulubu mtoto huyo akilia baada ya kutiwa nguvuni na polisi.
Na Gladness Mallya na Shani RamadhaniHII ni too much! Jalada namba KW/RB/7565/2014-SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI lililopo kwenye Kituo cha Polisi cha Kawe, Dar, linamhusu mama aliyetajwa kwa jina moja la Teddy, mkazi wa Tegeta kwa madai ya kumtumikisha na kumtesa mtoto Magdalena Elisha (10) na kumsababishia majeraha na makovu ya vidonda sehemu mbalimbali mwilini.
Mtoto Magdalena Elisha anayedaiwa kusulubiwa na mama huyo.
Kwa
mujibu wa Teddy, bila kujua kwamba ni kosa kumwajiri mtoto, aliamua
kumwadhibu mtoto huyo kutokana na kutomsikiliza bosi wake hasa
alipokuwa akionywa kuachana na tabia ambayo haikuwa ikimfurahisha.Kwa upande wake Magdalena alidai kwamba alikuwa akipokea kipigo kila siku hasa wakati mama huyo alipokuwa akirejea nyumbani kutoka ‘jobu’ na kukuta mwanaye analia.
“Alikuwa akinipiga kila siku akikuta mtoto (wa miaka miwili) analia. Pia kuna siku alinipiga sana asubuhi, nikaona nikimbilie kwa mjumbe, ndiyo tukaenda kituo cha polisi, tukakutana naye akiwa anatoka polisi kutoa taarifa kuwa nimepotea, mimi naomba nisaidiwe nirudi kwa mama yangu Arusha,” alisema Magdalena na kumfanya bosi wake huyo apewe kibako na vyombo vya sheria.