Wakati wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiendelea kujadili sura za rasimu ya Katiba mpya Mwenyekiti wa Bunge hilo SAMWEL SITTA amesema inatafutwa namna bora ya kuwawezesha wajumbe waliopo nje ya Bunge kwa sababu mbalimbali, wanaotaka kupiga kura, kupata haki hiyo wakiwemo wanaotarajia kwenda kwenye ibada ya Hija.
Kuhusu muda wa Bunge Mwenyekiti huyo amesema muda uliopangwa kukamilisha kazi ya kuandika Katiba inayopendekezwa unatosha, ambapo Kamati ya Uandishi inatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Septemba 21 mwaka huu kwa ajili ya kupigiwa kura na wajumbe wa Bunge hilo.
Wakati tukizipokea hizo taarifa, vyama vinavyounda UKAWA vimemtaka mwenyekiti wa bunge la katiba Samwel Sitta kushauriana na kamati ya uongozi kuangalia uwezekano wa kuahirisha bunge hilo sababu mchakato wa katiba hautoweza kufikia hatua za mwisho kwa wakati.
Mwenyekiti James Mbatia amesema kuendelea kwa bunge hilo hadi October 4 2014 ni kuhalalisha matumizi mabaya ya fedha.