Jumuiya ya Maendeleo ya Wanabusega (Budeco), imelaani tukio la kubakwa mwalimu wa shule ya Busega mkoani Simiyu.
Tukio
hilo lililotokea Agosti 23 mwaka huu, ambako majambazi wakiwa na silaha
walivamia nyumba ya Mratibu Elimu Kata, Samwel Mkumbo na kupora sh
milioni 18, kisha kuvamia chumba cha mpangaji ambaye ni mwalimu wa kike
na kumpora sh 50,000 na kumbaka.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi,
Mwenyekiti
wa Budeco, Massele Ginhu, alisema tukio hilo litarudisha nyuma
maendeleo ya elimu, kwa kuwa ni moja ya changamoto inayowakabili
wilayani hapo.
Alisema
kitendo hicho si cha kufumbiwa macho na wahusika watakaobainika,
wachukuliwe hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo vya kinyama na
kiuaji kwa watu wanaojitolea kufanya kazi ya kujenga taifa.
Aidha,
wanachama wengine wa Budeco walishauri serikali kujenga nyumba karibu
na mazingira ya kazi ili kulinda wafanyakazi na watumishi wa umma
wanaofanya pembezoni mwa miji.
Pia, walishauri ulinzi shirikishi kuboreshwa ikiwa ni njia ya kusaidia kulindana kwa watu wa maeneo yenye matishio ya uhalifu.
Na Asha Bani-Simiyu