1. UNA MATUMIZI MABAYA YA PESA
Wapo
watu ambao wanapopata pesa zinakuwa hazitulii kabisa mikononi mwao,
kila kitu kinachopita mbele ya macho yao kinakuwa halali yao.
Kama una tabia hii ya kufanya matumizi mabaya ya pesa elewa kabisa utaendelea kuishi maisha magumu na yale yale siku zote.
Jitahidi sana kudhibiti pesa zako na sio kudhibitiwa na pesa.
Kumbuka
unapotafuta pesa kuna muda ambapo unakuwa unatumia juhudi nyingi sana
mpaka kuzipata, kwanini sasa linapokuja suala la matumizi uzipoteze
kiurahisi tu, weka ulinzi kwenye pesa la sivyo utaendelea kukosa pesa
katika maisha yako kila mara
2. HUNA TABIA YA KUJIWEKEA AKIBA YA KUTOSHA
Hiki
ni kitu muhimu ambacho kinakufanya uendelee kukosa pesa. Kwa muda mrefu
umekuwa ukiishi maisha ambayo hujiwekei akiba ya kutosha ambayo
itakusaidia leo na baadae katika maisha yako.
Kama
una tabia hii ya kutojiwekea akiba utakwama na utashindwa hata
kuendesha miradi yako mwenyewe itakayokusaidia kuachana pengine na
kuajiriwa.
Jijengee
tabia hii bora ya kujiwekea akiba zako mwenyewe na kama huwezi hili au
unaona kama unashindwa hakikisha kwanza unajilipa mwenyewe hapo utapata
pesa ya kuweka akiba ya ziada.
3. UMEKUWA MUONGEAJI SANA
Mara
nyingi umekuwa mtu wa kuongea sana na sio kutenda hali hii imekuwa
ikikupunguzia mwendo wa kuelekea kwenye mafanikio na kujikuta unaendelea
kukosa pesa katika maisha yako.
Kama
unataka kufanikiwa na kuona ndoto zako zinatimia hakikisha unakuwa sio
mtu wa maneno, jifunze kuchukua hatua muhimu kwa kutenda. Tabia hii ya
kuongea sana ndiyo inayosababisha uendelee kukosa pesa katika maisha
yako kila wakati.
4. HUJAJIWEKEA VIANZIO VINGI VYA PESA
Umekuwa
ukikosa pesa mara kwa mara kutokana na kukosa vianzio vingi vya pesa
ambavyo vingekupatia pesa za kutosha na kukupa uhuru wa kifedha.
Unapokuwa na vianzio vingi vya pesa vitakusaidia wewe kusimama imara hata pale mambo yako yanapokwenda vibaya.
Unataka kuachana na hali hii ya kukosa pesa, tengeneza vianzio vingi vya pesa vitakavyokusaidia baadae kwenye maisha yako.
5. UNAFIKIRI SANA JUU YA KUSHINDWA
Mara
nyingi umekuwa ukiwaza vizuizi vinavyokuzuia kufanikiwa badala ya
kuchangamkia fursa zilizopo. Umekuwa ukiwaza sana nikiwekeza hapa
itakuwaje? au nitapata hasara? Kutokana na mawazo haya ni ukweli
usiopingika ni moja ya kitu ambacho kimekufanya uendelee kukosa pesa
katika maisha yako.
6. HUNA ELIMU YA KUTOSHA KUHUSIANA NA MAMBO YA PESA
Kutokana na kukosa elimu hii muhimu kwako, imekufanya uendelee kukosa pesa za kutosha kila kukicha.
Kumbuka hii ni elimu ambayo haifundishwi rasmi shuleni wala nyumbani lakini ni muhimu sana katika maisha yako kujifunza.
Jifunze juu ya mzunguko mzima wa pesa unavyofanya kazi na suala zima la ujasiriamali na masoko.
7. UNAFANYA KAZI SANA KWA AJILI YA PESA
Hii
ni sababu kubwa sana inayokufanya kila siku uendelee kukosa pesa.
Maisha yako yanazidi kuwa magumu kila siku kwa sababu unafanya kazi kwa
ajili ya pesa na matokeo yake unajikuta pesa inakufanya kuwa mtumwa kila
siku.
Jifunze
kutenda mambo yako kwa ubora wa juu na kwa viwango pesa zitakuja
zenyewe. Kama unafanya biashara fanya kwa ufanisi na ubunifu wa hali ya
juu, wateja watakuja wenyewe na utapata pesa za kutosha.
Acha
kabisa tabia ya kuitumikia na kuifukuza pesa katika maisha yako. Na
kama utaendelea kufukuza pesa, utashangaa katika maisha yako utakuwa mtu
wa kukosa pesa kila siku.
Unaweza
ukabadili na kufanya maisha yako vyovyote vile unavyotaka yawe kama tu
utaamua, hizo ndizo sababu muhimu zinazokufanya uendelee kukosa pesa
katika maisha yako.