Advertisement

Responsive Advertisement

AELEZEA JINSI ANAYOJIINGIZIA KIPATO CHA KUMTOSHA KWA CHUPA TUPU ZA MAJI


MKAZI wa Manzese, Kata ya Mafiga, Manispaa ya Morogoro, Oscar Philipo amemudu kuihudumia familia yake ya watoto wawili kutokana na biashara ya kuokota na kuuza chupa tupu za maji zinazomwingizia Sh 180,000 kila mwezi, imefahamika.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili juzi katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF) lililopo ndani ya Uwanja wa Jamhuri wa mjini Morogoro mara baada ya kupima afya yake, Banda la NHIF linatoa huduma za upimaji afya kwa wachezaji wa Shimiwi na wananchi wa mkoa huo.
Katika mashindano ya Shimiwi yanayoendelea kufanyika mjini hapa katika uwanja wa Jamhuri, Philipo amekuwa akiokota chupa nyingi tupu za maji baada ya zinazotumiwa na wachezaji.
Hivyo alisema, biashara ya kuokota chupa tupu za maji aliianza miaka mingi na kwamba kazi hiyo imekuwa ikimuingizia kipato cha kumudu kuendesha familia yake ya watoto wawili.
Mkazi huyo alisema, kutokana na tatizo la ajira, ameamua kujiajiri mwenyewe kwa kuokota chupa hizo ambazo kwa sasa zina soko kubwa Dar es Salaam na kwa siku ana uwezo wa kukusanya kilo 20 na kilo moja inauzwa Sh 300 hivyo kujipatia Sh 6,000 kwa siku.
“Kwa kiwango cha kufikisha kilo 20 kila siku ...ninapata makusanyo ya fedha Sh 180,000 kwa mwezi na zinanisaidia kuendesha familia yangu, ingawa mahitaji ya kila siku ni makubwa kuliko kipato kinachoingia,” alisema Philipo.
Hata hivyo alisema katika biashara hiyo anapata changamoto hasa kutoka wa vijana wanaobwia 'unga' mitaani wakati mwingine wanamkaba na kumwibia fedha.

Post a Comment

0 Comments