Advertisement

Responsive Advertisement

AUAWA KATIKA UGOMVI WA KULISHWA NYAMA YA PAKA HUKO MTWARA


Mkazi wa Mtwara Elias Edward amefariki dunia baada ya kupigwa na mchi kichwani katika ugomvi wa kulishwa nyama ya paka.
Kamanda wa polisi Mtwara alisema marehemu aliuawa na mwanaye Said Lukas ambaye ndiye aliyepika kitoweo hicho na kumpa baba na mama yake ambao hawakujua ilikua ni aina gani ya nyama.
Inasemekana mtuhumiwa huyo alikuta paka huyo ameuawa na watoto waliokua wanacheza kisha kumchukua na kwenda naye nyumbani ambapo alimchemsha vizuri na kuwatengea wazazi wake.
Baada ya kugundua ni paka ulizuka ugomvi mkubwa kati yao na baadaye mtuhumiwa kumvizia na kumpiga kichwani hadi kufa.

Post a Comment

0 Comments