Habari ya mjini kwa sasa ni bethidei ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutimiza miaka 26 tangu kuzaliwa, lakini ndani ya tukio hilo, mengine yameibuka!
Miongoni
mwa yaliyoibuka kwenye sherehe hiyo iliyofanyika Jumapili iliyopita
nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar es Salaam
ni madai ya mama Wema, Mariam Sepetu kudaiwa kupewa nafasi ya kutoa
‘neno la hekima’ lakini akaitumia kumvurumishia mitusi aliyekuwa shosti
wa Wema, Kajala Masanja.
Baada ya sherehe hiyo, Jumatatu na Jumanne, mitandao mingi ya kijamii ilitumbukiza video
yenye sauti ikimuonesha mama Wema akimrushia matusi Kajala kwa kile
kilichodaiwa kuwa ni kutokana na kukorofishana kwa mwanaye na Kajala
aliyewahi kumfadhili mahakamani kwa kumlipia faini ya shilingi milioni
13 asiende jela kwa kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa na zuio la kisheria.
Katika
kufuatilia sakata hilo, Amani lilinyetishiwa kwamba Kajala baada ya
kushindwa kuvumilia, ameamua kumshitaki mahakamani mama Wema.
Chanzo
chetu kinadai kuwa Kajala alifikia uamuzi huo baada ya kushauriwa na
familia sanjari na wafuasi wake (Timu Kajala) ambapo sasa, timu hiyo na
Timu Wema wameingia vitani tena.
“Kajala
ameshawasiliana na wanasheria wawili na kutoa maelezo yake, wao
wanaandaa faili ili mashitaka yafike mahakamani, amekasirika sana.
“Amesema mama Wema ametumia nafasi ya kukutana na watu kumdhalilisha bila kumpa nafasi ya kujitetea, ameona si sawa hata kidogo,” kilisema chanzo hicho ambacho ni jirani na Kajala.
“Amesema mama Wema ametumia nafasi ya kukutana na watu kumdhalilisha bila kumpa nafasi ya kujitetea, ameona si sawa hata kidogo,” kilisema chanzo hicho ambacho ni jirani na Kajala.
Katika
sauti, mama Wema anasikika akitamka matusi (hayaandikiki) huku Wema
naye anasikika akimsihi mama yake asimtaje jina Kajala kwa kuwa kufanya
hivyo ni kumpaisha. Hapa inamaanisha kwamba, Wema alitaka mama yake
afunguke lakini bila kutamka jina la mtu.
Katika hatua nyingine, mama Wema alisema kauli iliyoashiria kwamba Timu Kajala ilikuwemo ndani ya bethidei ya mwanaye. “Nasema haya huku najua humu ndani kuna Timu Kajala, lakini nasema….(matusi mazito)”
Baada
ya madai hayo yote, juzi, Amani lilimsaka Kajala kwa njia ya simu ili
kumuuliza ukweli wa madai hayo. Licha ya kutopokea simu ya mwandishi
wetu, alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno ‘SMS’ na kuulizwa kila kitu.
Hata
hivyo, badala ya kujibu alikaa kimya, baada ya dakika kama kumi na
tano alimrushia kwa simu mwandishi wetu video hiyo ambayo anadai
kutukanwa na mama Wema bila kusema chochote hali iliyotafsiriwa kuwa
kama alisema; ‘hebu oneni wenyewe jamani, nimemkosea nini mama Wema?’
Katika hatua nyingine siku hiyo, meneja wa Wema, Martin Kadinda alikuwa na kazi ya ziada kuhakikisha, mama Wema na mama Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ hawakai jirani au meza moja licha ya kwamba watoto wao wamependana.
“Kadinda
ana kazi ngumu sana, unajua anatakiwa kuhakikisha kwamba mama Wema na
mama Diamond hawakai meza moja. Sijui anaogopa nini, kwani hawa si watu
ambao watoto wao wana mpango wa kuoana?” alihoji mwalikwa mmoja.
Katika bethidei hiyo, Wema alizawadiwa magari mawili, Nissan
Murano lenye thamani ya shilingi milioni 36 alilopewa na Diamond na BMW
545i lenye thamani ya shilingi milioni 56, inadaiwa alizawadiwa na
Kadinda!
0 Comments