SHERIA iliyopitishwa na wakazi wa Arumeru mkoani Arusha
ya kuwachapa viboko 70 hadi 120 wasichana wanaovaa nusu uchi na
wavulana wanaovaa mlegezo, kuvuta bangi, wizi, matusi na ulevi nyakati
za kazi imeanza kufanya kazi baada ya kijana Zakayo Leonard (26)
kuchapwa viboko 120 kwa makosa mbalimbali likiwemo uchafu wa kutofua
nguo zake.
Kijana huyo mkazi wa Ilboru, alihukumiwa adhabu hiyo kwa kuchapwa
viboko 70 akidaiwa kutenda kosa la kumshambulia baba yake mzazi
aliyetambulika kwa jina la mzee Ng’uraa na kumng’oa jino moja.
Pia alitandikwa viboko 30 kwa kosa la kumtolea maneno machafu mzee wa
kimila (Laigwanani) na baadaye alicharazwa viboko 20 kutokana na tabia
ya uchafu wa kutofua nguo zake.
Hata hivyo, mara baada ya adhabu hiyo ya viboko 120 kwa mkupuo,
kijana huyo alizimia na kushindwa kuinuka wala kutembea hali
iliyolazimika kusaidiwa kwa kubebwa na morani wa Kimasai hadi nyumbani
kwake.
Adhabu hiyo ilitekelezwa hadharani mbele ya wazee wawili wa ukoo
(Laigwanani) waliokuwa wakishuhudia huku mtuhumiwa akitakiwa kutojigusa
popote wakati wa utekelezaji wa adhabu hiyo na kwamba iwapo angejishika
popote viboko hivyo alivyochapwa vingefutwa na kurejea upya.
Wazee wa makabila ya Wamasi, Waarusha na Wameru wamejiwekea utaratibu
wa kimila bila kujali kama unafuata maadili ya mwanadamu kwa kuwaadhibu
wahalifu hadharani bila kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
credits:gpl
0 Comments