Mgogoro mwingine mkubwa wa kifamilia wa kugombea maiti umeibuka mjini
Moshi na kusababisha mwili wa Rosemary Marandu kuhifadhiwa mochwari kwa
siku34.
Mwili wa marehemu huyo aliyefariki dunia Septemba4 umehifadhiwa
katika hospitali ya KCMC na umekua ukilipiwa shilingi 9,000 kila siku
hivyo siku34 gharama yake ni sh306,000.
Mama mzazi wa marehemu alisema mumewe aitwaye Flavian Marandu ndiye
anayeshikilia mwili huo hadi sasa bila kutoa sababu yoyote kutokana na
kushindwa kuelewana na familia yake.
Hata hivyo baba wa marehemu alisema habari hizo si za kweli na kwamba
mkewe anamzushia uongo kwani ameshindwa kuja kupanga taratibu za
mazishi.
0 Comments