Mbunge
wa Kawe, Halima Mdee na wenzake 8 jana wamepata dhamana katika Mahakama
ya Kisutu, Dar. Kesi yao kutajwa tena Oktoba 21, 2014.
Siku
ya jana washtakiwa hao walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi
Kaluyenda na kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali Mkuu,
Kangola aliwataja washtakiwa kuwa ni Mbunge wa Kawe, Mdee, Rose Moshi,
Penina Peter, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia Fanuel, Edward
Julius, Martha Mtiko na Beatus Mmari.
Mdee
na wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili la kwanza washtakiwa
wote wanadaiwa Oktoba 4 mwaka huu, Mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni,
walikaidi amri ya Ofisa wa Polisi SP Emmanuel Tillf iliyowataka
watawanyike.
0 Comments