Advertisement

Responsive Advertisement

PICHA ZA AJALI YA BASI LA NBS BAADA YA KUGONGA PUNDA MKOANI TABORA


Habari zilizotufikia  kutoka mkoani Tabora ni kwamba basi la NBS lililokuwa linatoka jijini ,Mwanza kwenda Mpanda,limegonga punda leo asubuhi na kupinduka katika eneo la Nzega Ndogo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia ni kwamba mtu mmoja,ambaye ni kondakta wa basi hilo amefariki dunia na majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Nzega.Inaelezwa kuwa majeruhi 12 wako mahututi

  TAIRI ZA MBELE ZA BASI HILO AMBAZO ZILICHOMOKA KUFUATIA AJALI HIYO. Picha na Kadama Malunde

Post a Comment

0 Comments