Mwanamke mmoja Kilimanjaro amekamatwa na polisi akidaiwa kumkata
mtoto wake mwenye umri wa miaka nane nyama ya paja na kuichoma mithili
ya mshikaki.
Mwananmke huyo aliyetajwa kwa jina la Dafrosa Massawe anadaiwa
kufanya unyama huo mwishoni mwa wiki na majirani wanasema mama huyo
alifanya hivyo akiwa amelewa.
Kamanda wa Polisi Kilimanjaro Koka Moita alisema mwanamke huyo
ataendelea kushikiliwa hadi uchunguzi wa tuhuma hizo utakapokamilika
kabla ya kupelekwa mahakamani.
Akizungumza na Gazeti la MWANANCHI katika hospitali ya Kibosho mtoto
huyo alisema hafahamu kosa alilofanya hadi mama yake ambaye ni
mtengenezaji wa pombe za kienyeji kumfanyia kitendo hicho.
Alisema mama yake alirudi nyumbani usiku na kumkuta amekaa na
kumsalimia kisha akamwomba chakula wakati akijua hakuna na baadae
aliingia jikoni na kuchukua kisu kisha kumkata nyama kwenye paja lake
baada ya kumwambia alishinda na njaa siku nzima.
Alisema baada ya kuikata aliichoma kama mshikaki na ilipoanza kufuka
moshi na kutoa harufu aliitoa jikoni na kumwekea mtoto huyo puani ili
avute harufu yake.
0 Comments