Katika hali isiyokua ya kawaida mwili wa Benadetha Steven mwenye
miaka 35 aliyefariki dunia juzi umefanyiwa matambiko ya kimila baada ya
kupasuliwa na wembe ukiwa kaburini na kuingizwa kuku ndani ya tumbo lake
ikiwa ni ishara ya kuondoa mkosi.
Tukio hilo lilitokea juzi katika mtaa wa Mapinduzi, Shinyanga wakati
waombolezaji wakiwa hatua ya mwisho ya kumzika marehemu lakini gafla
alijitokeza ndugu wa marehemu mwanamke na kuwazuia waombolezaji huku
mwenyewe akiingia kaburini na kufungua sanduku kisha kumchana tumbo
marehemu aliyekua akisumbuliwa muda mrefu na uvimbe tumboni.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kaka wa marehemu ambaye hakutaka
kujitambulisha jina lakini alikua kabila la Mkurya,aliupasua mwili wa
marehemu kwa kutumia wembe kisha kuweka kifaranga cha kuku tumboni
kikiwa hai na baadaye kufunika jeneza na kuruhusu maziko.
Walisema kabla ya tukio hilo kulitokea mabishano kati ya waombolezaji
na ndugu wa marehemu wakitaka afanyiwe matambiko katika hospitali ya
Mkoa wa Shinyanga alikokua akitibiwa.
“Mgogoro ulianzia nyumbani hata kabla ya kwenda makaburini,na wakati
mazishi yanaendelea ndipo ndugu mmoja akaingia ndani ya kaburi akiwa
amevaa mipira ya mikono ‘Gloves’ akiwa na wembe na boksi dogo lililokua
na kifaranga cha kuku na kuzuia waombolezaji wasitupe udongo kaburini.
Inasemekana ndugu wa marehemu waliamua kufanya hivyo wakiamini
wanaondoa mkosi ili kifo kama hicho kisitokee tena kwenye familia yao.
0 Comments