Mwanamke huyo mwenye miaka 67 ambaye awali alikuwa sista alipewa daraja hilo jumamosi iliyopita lakini upadrisho wake uliingia kwenye mzozo baada ya uongozi wa kanisa lake kudai hautambui kuapishwa kwake.
Lakini kwa upande wake alipingana nao na kusema haoni sababu za kukataliwa kuwa padri kwani Yesu alifundisha watu wote bila kubagua jinsia wala hadhi zao.
Ibada ya upadrisho iliongozwa na Askofu Bridget Mary Meehan wa Chama cha Mapadri wanawake wa kanisa Katoliki na wakati akipewa upadri hakuonyesha hofu yoyote mbali na tishio lakutengwa na kanisa.
0 Comments