Spika wa Bunge Anne Makinda
amesema sio kazi yake kuwasimamisha wenyeviti wa Kamati za Bunge ambao
wanatuhumiwa na ishu ya fedha za Escrow badala yake ni wao wenyewe
kujiondoa kama njia ya kutii maazimio yaliyopitishwa na Bunge ambayo
yanawataka kuwajibika.
“Azimio
linasema viongozi wa Kamati hizi watawajibika kwenye Kamati zao,
tusibadilishe maneno. Naona na gazeti lingine linasema
hawajajiuzulu, what is that? Suala la azimio kwamba viongozi hawa watatu
wa Kamati wajiuzulu”—Anne Makinda
Askari wawili wa kituo cha Ikwiriri,
Mkoa wa Pwani wameuawa na majambazi ambao idadi yao haijafahamika na
kupora bunduki tano, risasi 60 na mabomu mawili ya machozi jana.
“Walikuwa
ni majambazi wengi, walivamia na kuanza kuwashambulia askari wetu,
walifanikiwa kuwaua askari wetu wawili na kuchukua silaha… Jeshi la
Polisi nchini linalaani tukio hilo ni baya”– Advera Bulimba, msemaji wa Jeshi la Polisi.
Isikilize taarifa yote hapa niliyorekodi kwenye Habari ITV, bonyeza play.
0 Comments