. Kwa mara nyingine tena, taharuki, hofu na wasiwasi mkubwa viliwakumba wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa saa mbili baada ya kundi maarufu la waporaji la Panya Road, kuvamia mitaa mbalimbali na kupora mali.
Taarifa za kundi hilo lililopora watu katika
baadhi ya maeneo ya jiji hilo zilienea kwa kasi ya ajabu kupitia
mitandao ya kijamii watsap, twitter, jamii forum, blog, instagram na
ujumbe mfupi wa simu.
Baada ya maeneo ambako kundi hilo linadiwa kufanya
uporaji ni Tabata, Magomeni Kagera, Sinza, Mwananyamala, Kinondoni,
Kijitonyama, Manzese, Kigogo na Buguruni, huku wanafunzi wanaoishi
katika Hosteli za Chuo Kikuu Dar es Salaam, wakitoka nje ya mabweni yao
kwa kuhofia kuvamiwa na kikundi hicho.
Taharuki hiyo iliyoanza saa mbili usiku,
ilisababisha wakazi wa maeneo mengi ya jiji kujifungia ndani, huku
wafanyabiashara wakifunga maduka na kujificha wakihofia kundi hilo la
wahalifu.
Imeelezwa kuwa fujo zilianzia mchana baada ya kiongozi wa Panya Road aitwaye Diamond kuuawa maeneo ya mpakani mwa Tandale na Mwananyamala darajani usiku wa kuamkia mwaka mpya kwa kukatwakatwa na mapanga.
Baada ya kumzika mwenzao JANA, vijana hao wakajipanga kwa ajili ya kufanya fujo.
Usiku ulipoingia wakaanza kazi na kusababisha taharuki kwa wakazi wa Jiji la Dar.
Baadhi ya mashuhuda walioshuhudia matukio hayo wanadai vijana hao walikuwa na silaha mbalimbali yakiwemo mapanga na walivamia maeneo kadhaa zikiwemo baa.
Wateja waliokuwa katika baa ya Calabash iliyopo maeneo ya Mpakani, Mwenge walilazimika kuacha vinywaji vyao na kukimbia hovyo huku wengine wakikanyagana na kukatwa na vipande vya chupa kwa kile kilichodaiwa kuwa vijana hao walikuwa wanakatiza maeneo hayo japo hawakuingia ndani.
Baada ya tukio hilo wateja wengi waliamua kurudi majumbani kutokana na baadhi yao kujeruhiwa na vipande vya chupa wakati wakikimbia.

0 Comments