Mshindi wa tuzo ya Mchezaji bora wa dunia mara nne Lionel Messi hataihama klabu yake ya Barcelona kama ilivyoanza uvumishwa kwenye baada ya magazeti barani ulaya baada ya kuthibitisha kuwa ataendelea kubaki na klabu yake ya Barcelona kwa muda mrefu zaidi.
Kwa mujibu wa gazeti la michezo nchini Hispania la Mundo Deportivo, Messi ambaye ni nahodha wa pili wa Barcelona hataihama klabu hiyo na badala yake ataendelea kucheza hapo kwa miaka mingi zaidi kwa klabu hiyo ni kama nyumbani kwake .
Tayari matajiri wa kiarabu na kirusi wanaomiliki klabu za Paris St Germain na Chelsea walishaanza mipango ya chini chini ya kumsajili nyota huyo kwenye klabu zao baada ya kufahamishwa kuwepo kwa hali ya kutoridhika kwa nyota huyo ndani ya klabu yake .
Tajiri wa Chelsea Roman Abramovich alikuwa anafanya mpango ambapo alikmhusisha nyota wa zamani wa Barcelona Cesc Fabregas ambaye ni rafiki wa karibu wa Messi akimtaka nyota huyo Mhispania kusaidia kumsaidia kumshawishi Messi kuhamia London .
Katika mpango huo pia alihusishwa mpenzi wa Fabregas Daniella Seeman ambaye ana ukaribu na mpenzi wa Messi na katika majaribio yote hayo hakuna aliyeweza kufanikiwa kuwa na ushawishi wa nguvu kwa Messi.
Nasser AL-Khelaifi ambaye ni tajiri wa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa akiiwakilisha familia ya kifalme ya nchini Qatar ambao ndio wanaimiliki klabu hiyo bingwa ya Ufaransa naye alikuwa anaandaa ofa ya kumnunua Messi kwa kiwango chochote kile cha fedha ambacho Barcelona wangetaka endapo wangekuwa tayari kumuuza .
Messi ameichezea Barcelona tangu akiwa na umri wa miaka 13 na amekuwa wazi kutamka kuwa Barcelona ndio klabu pekee ambayo ataichezea maisha yake yote akiwa ulaya .
Hivi karibuni kumekuwa na tetesi nyingi kuhusiana na nyota huyo kuwa na maisha yasiyo na raha ndani ya Barcelona hali ambayo hata hivyo uongozi wa klabu hiyo umekuwa mstari wa mbele kukanusha .
0 Comments