Deogratius Mongela na Chande Abdallah
MATUKIO ya
mateso, unyanyasaji na utumwa kwa watoto yanashika kasi nchini! Safari
hii mwalimu wa shule moja ya msingi iliyopo Mburahati jijini Dar
aliyetajwa kwa jina moja la Lucy ametia aibu baada ya kutiwa mbaroni
katika Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar akituhumiwa kumtumikisha mtoto
mwenye umri wa miaka 12 aitwaye Sakina kwa kumuuzisha mayai ya
kuchemsha na soseji.
Mwalimu huyo akijitetea juu ya sakata hilo.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wetu, tukio hilo lilichukua nafasi maeneo ya
Kashuda Bar, Magomeni hivi karibuni baada ya wakazi wa eneo hilo
kuhamaki kumuona binti huyo akitembeza mayai na soseji mtaani wakati
umri wake ni mdogo kinyume na sheria za ajira.
RAIA WAMZUNGUKA
Ilisemekana
kwamba, baada ya kukerwa na kitendo hicho huku Sakina akionekana hana
furaha, raia hao wenye hasira kali walimhoji ambapo alimtaja mwalimu
huyo kuwa ndiye bosi wake aliyemchukua kutoka Tanga kwa ajili ya kufanya
kazi za ndani (hausigeli).
AFUATWA SHULENI
Ilidaiwa
kwamba, wakifuatana na mtoto huyo, wakazi hao walifunga safari hadi
shuleni kwa mwalimu huyo Mburahati ambapo wanahabari wetu walitonywa na
kutia timu hadi kwa mkuu wa shule hiyo, Kibassa ambaye alikiri
kuchukizwa na kitendo cha mfanyakazi wake kumwajiri mtoto wa miaka 12
kumtumikisha kazi akiwa ni mwajiri wa serikali.
“Kimsingi
nimesikitishwa kwa sababu Lucy ni mwajiriwa wa serikali, hapaswi
kufanya jambo baya kama hili. Kwa umri wake alipaswa awe darasani,”
alisema Kibassa.
MWALIMU AJITETEA
Kwa
upande wake, Lucy alijitetea kuwa binti huyo aliletewa na mtu
aliyemtaja kwa jina la Kizito aliyemuagiza mfanyakazi wa ndani, lakini
baada ya kufika binti huyo alimkataa na kudai bado mdogo asingeweza
kufanya kazi za ndani.
Mwalimu
huyo alisema alikuwa akimsubiri binti mwingine mkubwa aletewe na Kizito
ili amrudishe Sakina kwao na kudai kuwa hata biashara ya mayai
hakumtuma yeye bali alimtuma John (kijana wake wa kazi) ila inawezekana
Sakina alijiingiza kujisaidia na ugumu wa maisha.
Mwalimu huyo akiwekwa kikao.
BINTI ASIMULIA
Akiwa
shuleni hapo, mbele ya bosi wake, Sakina alifunguka kuwa amekuwa
akifanya biashara hiyo na kufanya kazi za ndani kwa Lucy huku akisimulia
kunusurika kubakwa na kupitia mateso mengine kama kunyimwa chakula na
kulazimika kutembeza mayai na soseji mchana kutwa.
“Nafanya
kazi za ndani na kutembeza mayai, kuna kaka mmoja nilimwomba msaada ili
nirudi nyumbani, akanilazimisha tufanye mapenzi ndipo anisaidie,
nilipokataa akaniacha,” alisema Sakina.
Hata
hivyo, mwalimu huyo alitolewa shuleni hapo chini ya ulinzi mkali kisha
kufikishwa Polisi Magomeni katika dawati la jinsia kwa hatua zaidi.
Credit:Global
0 Comments