Jokofu
Inasemekana vichanga hivyo vinakadiriwa kuwa
na umri wa mwezi mmoja,na miili hiyo iligunduliwa na rafiki wa mwenye
nyumba walikokutwa vichanga hivyo,ambaye alielekea jiji la Johannesburg
kwenye maziko ya mpenzi wake.
Anita King, msaidizi wa ndani
alitakiwa na mwajiri wake aifanyie usafi nyumba yake na wao wanaelekea
mazikoni,na Anita alipokuwa katika utekelezaji wa kazi hiyo,akagundua
haruku kali ikiingia puani mwake ikitokea katika jokofu la nyumba hiyo.
Naye
akadhani labda nyama imeharibika katika friji hilo,na anaeleza ilikuwa
ni harufu kali na nzito,na akahisi pengine hayo yamesababishwa na
kukatika kwa umeme nchini humo,hivyo akaamua kulifanyia usafi friji hilo
na sehemu ya kugandishia.
Anita anasema,ndani ya jokofu hilo nikakuta mfuko mkubwa wa plastiki wa kuhifadhia taka.
Na
mara nlipoufungua mfuko huo nilikumbana na harufu kali mno na mara
ikasambaa katika nyumba yote na hata nje ya nyumba pia.sikuyaamini macho
yangu anasema Anita niliona kijimkono na kichwa cha mtoto
mchanga.sikuwahi kuona kitu kama hiki maishani mwangu anasema Anita .
Wakati
wa msiba wa mpenzi wa mwajiri wake! Wageni walikuwa wakipewa mahitaji
ya chakula kutoka katika jokofu hilohilo na masalia ya vyakula
yalihifadhiwa katika jokofu hilo.
Hata hivyo majirani wanawaelezea wenye nyumba hiyo mahali ambako maiti hizo zilikutwa kuwa ni wacha Mungu na wapenda watoto.
0 Comments