
Siku
zote unapopita kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa kuna ukaguzi mkubwa
ambao kila abiria huwa anafanyiwa kabla ya kuingia kwenye ndege ambapo
hulazimika kuvua saa yako, kuziweka simu pembeni na vitu vingine ikiwemo
kuvua viatu na mkanda kabla ya kupita kwenye mashine maalum ya ukaguzi.
Hii imetoka Russia kwenye uwanja wa ndege
wa Pulkovo ambapo abiria mmoja aliekerwa na ishu ya Askari kusachisachi
kwenye mashine maalum yenye mfano wa mlango, aliamua kuvua nguo zote
baada ya kukasirishwa na hilo zoezi.

Maamuzi
ya kuvua hizo nguo ni ili kuwapa askari urahisi wa kufanya ukaguzi
ambapo aliwaacha hoi Wafanyakazi wa uwanja wa ndege na abiria wengine
pia huku Polisi wakiwa kimya bila kuzungumza chochote akapita zake.
0 Comments