Miezi minne iliyopita, Demeteriya
Nabire aliliwa na mamba alipokwenda mtoni karibu na makazi yake kuchota
maji.
Mnyama huyu alirudi tena baaae katika eneo lilelile na kumkuta
mume wa Nabire anasubiri, tayari kwa kulipa kisasi.
Demeteriya
Nabire alikuwa kwenye kingo za mto akiwa na wanawake wengine kutoka
kwenye Kijiji anachoishi, walikuwa wakichota maji kutoka katika Mto
Kyoga nchini Uganda, Mamba alifika na kumnyaka,alimburuza kisha
mwanamama huyu hakuonekana tena.
Mumewe, Mubarak Batambuze,
aliingiwa na hofu sana,Nabire alikuwa mjamzito.hivyo Mubarak hakupoteza
mkewe tu bali kiumbe kilichokuwa tumboni.alijihisi kukosa nguvu, lakini
Mwezi uliopita akasikia kuwa Mamba amerejea.
''Mtu mmoja akaniita 'mubarak nina habari kwa ajili yako, Mamba aliyemchukua mkeo amerudi, tena'
Mvuvi
huyo mwenye umri wa miaka 50 akaelekea mtoni na marafiki zake
.''alikuwa mkubwa, na tulijaribu kupambana nae kwa mawe na fimbo lakini
hatukufanikiwa''.alisema.
Hivyo Batambuze alienda nyumbani kwa muhunzi.
''nikamweleza
kuwa napambana na Mamba ambaye amenichukulia mke wangu na mtoto
aliyekuwa tumboni.ninataka sana kulipa kisasi,kisha nikamwambia
anitengenezee silaha ambayo ingeweza kumuua mamba huyo.
Mtu huyo alitaka nilipe kiasi cha pauni 3.20 ili atengeneze Mkuki.
Akiwa na mkuki wake mkononi alielekea kwenye mapambano.
Lakini
alipofika kwenye maji, Mamba alikuwepo eneo hilo, lakini Marafiki wa
Batambuze waliingiwa hofu na kumsihi asimshambulie kwa kuwa alionekana
mkubwa sana na angeweza kumla,wakamwambia kuwa Mkuki huo hautafaa.
Batambuze
akasisitiza waendelee kubaki, ''nilishindwa kumuua mwanzo, alisema,
''sioni tatizo nikifa wakati namuua Mamba natatumia mkuki huu, na
nitahakikisha amekufa''.
Ofisa wa wanyama pori Oswald Tumanya, amesema kuwa Mamba alikuwa na urefu wa zaidi ya mita nne na uzito wa kilo 600.
''nilikuwa na wasiwasi sana lakini kilichonisaidia ni Mkuki''alisema Batambuze.
Alifunga
kamba kwenye kwenye mkuki kwenye sehemu iliyotengenezwa mithili ya kisu
kikali, ''niliweka silaha yangu eneo Mamba alipo huku marafiki zangu
wakinisaidia kurusha mawe na kumchapa mamba mgongoni kwake wakitumia
fimbo, Alijaribu kunyanyua mdomo wake juu ili anishambulie.''
alishikwa
na hasira sana, kisha kulikuwa na hofu sana katika eneo hilo, lakini
nilikuwa na nia, na sikuhofu kufa, nilitaka kumuua hivyo nilirusha
silaha yangu alipo mamba kisha nikavuta kamba. Mamba alianza kuwa
matatani''.
Ilichukua saa moja na nusu mwa Batambuze na marafiki zake,wakipambana na Mamba, hatimaye alikufa
Wakiwa
wamechoka walirejea kijijini kwao ''kulikuwa na mshtuko mkubwa,
kilichomshangaza kila mtu ni ukubwa wa Mamba, hakuwa mamba wa kawaida,
alikuwa mkubwa sana .
Na Watu wakatuita mimi na marafiki zangu
mashujaa''alisema.
via>>BBC
via>>BBC
0 Comments