Tunda Man
Kwenye zile zilizosikika leo February 19 kwenye 255 ishu ya kwanza ni story ya mastar wawili Bongo Flevani, Matonya na Tunda Man, ishu iliyokuwepo ni wawili hao kutoelewana kwa muda mrefu.
Matonya
Tunda Man amesikika
kwenye 255 leo, amesema ni kweli hawakuwa na maelewano kwa muda mrefu
japo mwanzo walikuwa marafiki sana na walifanya kazi pamoja lakini
tofauti zao zilitokana na kazi.
Tunda amesema ameshiriki kwenye maandalizi ya album ya Matonya ‘Vaileth’ kwa 90%.
Mbunge Zitto Kabwe
Kulikuwa na story za kuvunjika kwa kundi la Kigoma All Star ambao tayari wameshafanya pamoja ngoma mbili na zikashika sana, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
amesema hakuna ukweli kwenye story hiyo, kundi hilo walikuwa na mipango
mingi kwa pamoja ikiwemo kufungua Saccos ambayo ingewasaidia kufanya
kazi zao kwa urahisi kwa kuwa ni ngumu kusupport wasanii wote 14.
Zitto
amesema kulitokea matatizo kadhaa ambayo yalifanya kutokamilika kwa
mipango hiyo ila kwa sasa kila kitu kitakuwa sawa kabla ya kufika kwa
kipindi cha uchaguzi Mkuu mwezi October.
Ili uweze kuzisikiliza story zote bonyeza play hapa.
0 Comments