STAA wa
filamu Bongo, Kajala Masanja kupitia kampuni yake ya Kay Intertainment,
ameamua kuungana na mastaa kibao Bongo katika kutokomeza mauaji ya watu
wenye ulemavu wa ngozi ‘Albino’ yaliokithiri hivi sasa.
Akichezesha taya na Uwazi, Kajala na timu yake nzima wameunda kitu
kinachoitwa ‘Simama Nami’ ambapo tayari wameshatunga wimbo wa pamoja
walioshirikiana na Mwasiti, Shilole, Linah, Keisha, Zamaradi, Kadjanito
na wengine wengi.
“Kwa kweli mauaji hayo yananiumiza kila kukicha, nilifikiria tutafanya
nini hivyo nikaona bora tufanye hii kampeni ambayo naamini mimi na
wenzangu tutafanikiwa. Kampeni hii si ya leo tu bali ni endelevu,”
alisema Kajala.
0 Comments