|
Habari
kutoka mkoani Mbeya zinasema kuwa watu zaidi ya 18 wamefariki dunia
papo hapo baada ya Hiace waliyokuwa wanasafiri nayo kupata ajali katika
eneo la uwanja wa ndege Kiwira wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya.
|
Gari hiyo imetumbukia katika mto wa Kiwira,wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
Mpaka
sasa Miili ya watu 22 imefanikiwa kutolewa kwani Hiace ilitumbukia
mtoni ambapo miili mingine imenaswa na juhudi za kuitoa
inafanyika.Katika jali hiyo inasemekana watu wawili tu ndiyo wamepona
akiwemo kondakta.
0 Comments