Askofu
Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali
Pengo, anatarajiwa kuongoza misa ya Ijumaa Kuu, itakayofanyika katika
Kanisa la Mtakatifu Joseph jimboni humo.
Wakristo wote duniani hufanya misa hiyo kila mwaka, kukumbuka mateso na kufa kwa Yesu Kristo.
Ratiba
iliyotolewa Dar es Salaam jana na Katibu wa Jimbo, Dennis Wigirwa
ilionesha kuwa Pengo ataadhimisha misa hiyo kanisani hapo itakayoanza
saa 9:00 jioni.
Pia, alisema kuwa Misa ya mkesha wa sikukuu ya Pasaka, itafanyika saa 2 usiku Jumamosi na Askofu huyo ndio atakayeiongoza.
Aliongeza kuwa misa ya Pasaka ya kukumbuka kufufuka kwa Yesu Kristo. itafanyika saa 3:00 asubuhi na itaongozwa na Pengo
0 Comments