Lulu akiwa kwenye pozi..
Lusekelo Samson Mwandenga (Secky) enzi za uhai wake
Msanii wa filamu machachari na mwenye vituko Elizabeth Michael (Lulu)
anadaiwa kupatwa na msiba wa mtu anayesemekana kuwa alikuwa ni mpenzi
wake.
Lulu ambaye ni nyota wa filamu ya “Foolish Age” anahusishwa kuwa alikuwa
akitoka kimapenzi na kijana huyo mfanyabiashara anayejulikana kwa jina
la Seki, chanzo kimoja kilieleza.
kwa mujibu wa chanzo hicho ni kwamba marehemu Lusekelo Samson Mwandenga (Secky) alikuwa na mkewe
mchaMungu, inasemekana amefariki kama alivyofariki Steven Kanumba miaka
mitatu iliyopita, ambaye naye alidaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na
mrembo huyo wa bongo movie.
Yapo madai kuwa vifo hivyo vinatokana na ushirikiana.
Kwa sasa Lulu ni mjamzito lakini hajamtaja mwanaume aliyempa ujauzito.
Na jana ilikuwa siku ya kuzaliwa ya Lulu.
Lemutuz kwenye ukurasa wake wa Instagram aliandika chanzo cha kifo chake kama inavyosomeka hapo juu.
FAMILIA YA MAREHEMU INASEMAJE?
Najua kama unafatilia habari zinazoendelea mjini utakua umekutana na taarifa ya kifo cha huyu ndugu yetu inaweza kuwa imekufikia lakini sio kwa usahihi, au chanzo cha kifo kinaweza kuwa kimepotoshwa na kuzua utata.
Sasa familia ya Marehemu Lusekelo Samson Mwandenga (Secky) imekanusha taarifa zinazoendelea kusambazwa kupitia voice note na kwenye mitandao kuhusu chanzo cha kifo chake na kwamba alikwenda kwenye birthday, ukweli ni kwamba aliumizwa na kiti cha kioo akiwa kambeba mtoto wake nyumbani kwake, akapelekwa hospitali na baadae akafariki akiwa Hospitali, hakuna kingine zaidi ya hapo.
Secky alikuwa rafiki wa watu wote wakiwemo wasanii wengi wa Bongofleva na hata Bongomovie pia ndio maana msiba huu umewagusa kutokana na ukarimu wake kwao akiwemo Wema Sepetu ambaye amesema >>> ‘Ulikua mtu wa watu, sanaaaaa…… najua utaliliwa na wengi…. they say vizuri havidumu, pumzika kwa amani baba…. It’s jus too hard to sink in….‘
Diamond Platnumz ameandika ‘Gone too soon my Brother… i still don’t wanna believe that you are realy Gone….dah si jana tu tumezungumza’
0 Comments