Jeshi la Polisi wilayani
Kahama mkoani Shinyanga limefanikiwa kuwakamata watu 6 na tuhuma za
kukutwa na viungo vya Albino wakiwa katika harakati za kuviuza viungo
hivyo.
Mkuu wa kituo cha Polisi wilayani Kahama Leonard Nyandahu,
amesema watu hao wamekamatwa jana majira ya saa 7 mchana katika nyumba
ya kulala wageni ya MAJI HOTEL, iliyopo Phantom kata ya Nyasubi
wilayani Kahama.
Nyandahu amewataja watu
hao kuwa ni Bahati Kirungu(56) mwalimu wa shule ya msingi Katungulu kata
ya Wendele,Mhoja John(24) mkulima mkazi wa Isagehe Nzega,Bilia
Busanda(39) mkulima mkazi wa Mogwa Nzega.
Wengine ni Shija
Makandi(60) mkulima mkazi wa Isagehe Nzega,Regina Kashinje(40) mkulima
mkazi wa Isagehe Nzega,na Aboubakary Ally(25) ambaye ndiye
aliyewahifadhi watu hao mkazi wa Isagehe Nzega.
Nyandahu amesema mnamo
tarehe 19.5.2015 asubuhi mkuu wa upelelezi kituo cha Polisi Nzega
alipata taarifa za mtu kuwa anauza viungo vya Albino na mtego wa
kumkamata ulifanyika bila mafanikio badala yake akahamishia biashara
hiyo wilayani Kahama.
Aidha Nyandahu amesema
maafisa upelezi mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na Afsa upelelezi kituo
cha polisi Kahama walifuatilia nyendo za watu hao na ndipo mtego wa
kuwakamata watu hao ulipowekwa na kuwanasa.
0 Comments