Msichana
Judith Chomile (15) amekiri kumnyonga hadi kufa mtoto mwenye umri wa
miaka 9 ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Bernard Benderi aliyejulikana kwa
jina la Edrini Mafuele baada ya kukorofishana wakiwa nyumbani kwao Kola Hill mjini Morogoro.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amesema msichana
huyo alimnyonga mtoto huyo siku ya Jumatano baada ya kutokea
mabishano kati ya marehemu na mtuhumiwa.
Amesema marehemu alikuwa akimtuhumu dada yake
kumuibia soksi za shule huku akimrushia maneno ya kejeli ndipo mtuhumiwa
akachukua uamuzi wa kumsukuma marehemu.
Amefafanua kuwa baada ya marehemu
kudondoka sakafuni mtuhumiwa alimbeba kumpeleka chumbani kisha kumnyonga
kwa kutumia kamba ya gauni na kusababisha kifo chake.
0 Comments