STAA mkongwe wa sinema
za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ ametoa ushuhuda mzito (confession) baada
ya kukiri kuishi maisha ya starehe ikiwemo unywaji pombe na kukosea
mwanaume sahihi wa maisha kwa kuingia kwenye uhusiano tofauti jambo
aliloliita ni ‘kumtumikia shetani kwa pombe na ngono’.
Staa mkongwe wa sinema za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’.
Akizungumza kwa njia ya
simu na mwandishi wetu hivi karibuni katika mahojiano maalum, Mainda
ambaye kwa sasa ni mlokole wa ‘tuimbe na kusifu’ aliweka wazi kuwa
kipindi cha nyuma, shetani alimzidi nguvu kwa kujichanganya maeneo ya
baa na kunywa pombe jambo ambalo kwa sasa kila akikumbuka huishia
kusikitika.
Alisema, kwa sasa hana
mpenzi na kwamba hatafuti lakini anamngojea yule ambaye anaamini atatoka
kwa Mungu kwa wakati muafaka.Mainda aliweka wazi kuwa anamshukuru Mungu
kwa kumuongoza katika njia nyoofu huku akiainisha kuwa maisha bila ya
kuwa na Mungu ni ya ajabu sana.
“Kwa kweli maisha ya
zamani yalikuwa ya ajabu, ulevi wa pombe, kutoka na wanaume tofauti
nikidhani ndiye mwanaume sahihi, zilikuwa ni nguvu za shetani,
namshukuru Mungu kwa kunibadilisha kwa kiwango hiki kwani nilimtumikia
sana ibilisi kwa mambo machafu, viongozi wangu wa dini wananipa mwanga
mkubwa mno juu ya Neno la Mungu na kila nikikumbuka maisha ya nyuma,
huwa siyatamani kabisa,” alisema Mainda.
0 Comments