Vurugu kubwa zimetokea katika mji wa
Njombe mkoani Njombe baada ya Basili Mwalongo mkazi wa mkoani humo
kuuawa kwa kupigwa na polisi jana usiku ambapo wananchi wameandamana
katika hospitali ya mkoa wa Njombe ambapo polisi wamelazimika
kuwatawanya kwa risasi na kujeruhi wananchi kadhaa huku baadhi ya maduka
yakifungwa na shughuli kusimama.
Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia
wananchi wakiwa wameandamana na kufunga barabara huku wakiwasha matairi
barabarani wakiwa wameshika chupa za maji kukabiliana na mabomu ya
machozi ambapo amezungumza na majeruhi kadhaa wa kadhia hiyo Fredy Sanga
akiwa amejeruhiwa kwa kupigwa risasi sehemu za siri na Lupiana Mandela
aliyejeruhiwa kichwani.
Diwani wa kata ya Njombe mjini Bw. Agrey
Mtambo aliyejaribu kuwatawanya wananchi hao bila mafanikio amesema
purukushani kati ya polisi na wananchi ambapo polisi walianza kutumia
silaha za moto.
Kufuatia vurugu hizo polisi mkoani
Njombe wamelazimika kupiga mabomu ovyo kutawanya mikusanyiko ya watu
huku kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Franco Kibona akigoma
kuzungumza na waandishi wa habari kwa madai kuwa hawezi kuzungumza
wakati vurugu zikiendelea halikadharika madaktari katika hospitali ya
mkoa wa Njombe wakigoma kuzungumza.
0 Comments