Kila
mtu ana ndoto na mtu ambaye anamhitaji awe mpenzi wake kwa maisha yote,
sio ajabu mtu akawa na ndoto za kumuwaza mtu ambaye ni ngumu sana
kwenye mazingira ya kawaida kuonana nae, pata picha ya huyu jamaa ambaye
yeye macho na akili yake ni kwa Malia Obama.
Kiprono Matagei kazi yake ni wakili Kenya, ndoto yake ni yeye na Malia Obama damdam,
alianza kumpenda tangu mwaka 2008.. moyoni mwake akaweka ahadi kwamba
hatokuwa na uhusiano na mwanamke yoyote mpaka siku ampate Malia wake !!
Jamaa kajiongeza kabisa, amesema mahari aliyopanga kutoa ni hii>>> ng’ombe 50, kondoo 70 nambuzi 30.
Kiprono kasema yuko serious kabisa na aliwashirikisha familia yake, wako tayari nao kumsaidia mpaka afanikiwe !!
Obama atakuwa
Kenya mwezi wa saba, ziara yake haitachukua muda mrefu lakini jamaa
amesema atajitahidi aitumie nafasi hiyo hiyo kumuona ‘baba mkwe huyo
mtarajiwa’ !!
0 Comments