Mbunge wa Jimbo la
Shinyanga mjini, Stephen Masele (kulia) akisalimiana na Naibu waziri wa
fedha nchini, Mwigulu Nchemba muda mfupi mara baada ya (Nchemba)
kuwasili katika ofisi za CCM Shinyanga mjini, wakati Nchemba alipokuwa
akitafuta wanachama wa CCM wa kumdhamini. Kulia mwanzoni ni mmoja wa
wajumbe wa kamati ya siasa, Rajabu Abasi -Picha na Suleiman Abeid
Mbunge wa Jimbo la
Shinyanga mjini, Stephen Masele ametoa ufafanuzi kuhusiana na madaiya
kumuunga mkono mmoja wa makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM),
wanaowaniakugombea urais kwa tiketi ya CCM na kukanusha habari
zilizoandikwa nabaadhi ya vyombo vya habari vilivyodai amejiunga kwenye
kambi ya MheshimiwaEdward Lowassa.
Masele ambaye pia ni
Naibu waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) alitoaufafanuzi
huo juzi alipokuwa akimkaribisha kada mwingine wa CCM, MwiguluNchemba
aliyefika katika ofisi za CCM Shinyanga mjini kwa ajili ya kutafutawana
CCM wa kumdhamini ili aweze kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM.
AkifafanuaMasele alisema
yeye kama mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini ni wajibu wake pamojana
viongozi wengine wa CCM wilayani humo kuhakikisha wanamsaidia kada ye
yotewa chama anayekwenda kwa ajili ya kutafuta wadhamini na hakuna mtu
anayemuunga mkono miongoni mwa waliotangaza nia ya kugombea urais kwa
vile
wote ni wake.
“Sisi kama wajumbe wa
kamati ya siasa ni wajibu wetu kuandaa mazingira mazuri kwa watangaza
nia wetu na makada wenzetu wote wanaokuja katika eneo letu hili, na mimi
kama mbunge ninao wajibu kabisa wa kushiriki kikamilifu kuhakikisha
kwamba mambo yote yanakuwa sawasawa, nawapongeza wale wote mliojitokeza
kumdhamini pia mwenzetuMwigulu Nchemba,”.
“Sisi huku wengine siyo
wajumbe wa NEC na walasiyo wajumbe wa Kamati kuu, lakini ni wajumbe wa
mkutano mkuu wa CCM Taifa, kazi yetuni kusubiri vikao vya juu vya chama
vifanye kazi yake na hatimae vitatuletea mgombea wa CCM na tutapigana
kufa na kupona kuhakikisha chama chetu kinashinda,”alieleza Masele.
Kwa upande wake kada wa
CCM na Naibu waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza na wanachama
wa CCM 45 waliojitokeza kumdhamini wakiwemo wazee maarufu wa mjini
Shinyanga alisema moja ya lengo lake kuu la kutaka kugombea nafasi ya
urais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuwavusha watanzania kuelekea
katika taifa lenye uchumi wa kati.
Mwigulu alisema anaamini
mgombea wa CCM ndiye atakayeibuka na ushindi mkubwa katikauchaguzi mkuu
wa Oktoba 25, mwaka huu na kwamba wanachosubiri watanzania walio wengi
hivi sasa ni kuona chama chake kinampa ridhaa ya kupeperusha bendera
yaCCM ili waweze kumchagua.
“Vyanzo vyangu vya
habari na taarifa mbalimbali zinaonesha watanzania wengi wanasubiri
chama changu kinipe ridhaa ya kupeperusha bendera ili wao waweze kuunga
mkono agenda yao waliyoiona tangu nilipotangaza nia ya kugombea urais,
sina mashaka ndani ya chama na nje ya chama kwamba agenda ya watanzania
ikishindanishwa na jambo lolote itashinda tu,”
“Kwa wana CCM, CCM
inapata uhalali wa kuongoza taifa letu kwa aina tatu ikiwemokutoka
urithi wa vyama vilivyokomboa taifa letu, pili kwa kazi ilizozifanya
kwakuunda serikali tangu ilipoanzishwa mpaka hivi sasa na kazi
zakuliletea taifa hili maendeleo tangu ilipoanzishwa mpaka hivi leo, na
pia sifa yatatu ni kwa kazi inazotarajia kwenda kuzifanya sasa,”
alieleza Nchemba.
Aidha kada huyo wa CCM
alirejea kauli zake za awali kwa kueleza kuwa moja ya agenda yakekuu
atakapofanikiwa kuingia Ikulu ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kipato
chakati pamoja na watanzania wenyewe kuwa watu wa nchi ya kipato cha
kati na waondokane na kauli ambayo wameisikia muda mrefu ya uchumi kukua
huku wao wakiona umasikini ndiyo unaokua.
Katika hatua nyingine
Mwigulu alikanusha madai kwamba kitendo cha kujitokeza idadikubwa ya
makada wa CCM kutaka kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania itakuwa ni chanzo ya chama hicho kusambaratika baada ya majina
yamakada wengi kukatwa wasiweze kugombea nafasi hiyo.
“Si kweli kwamba eti CCM
itasambaratika mara baada ya uteuzi wa mgombea wake katikanafasi ya
urais wa Jamhuri ya Muungano, tupo imara na tutaendelea kuongoza
nchihii, hatuwezi kusambaratika, maana watanzania hawataangalia sura ya
mtu,wataangalia agenda kuu watakayoisimamia ili kuifanya nchi kuwa ya
uchumi wakati,” alieleza Nchemba.
Aidha alitoa wito kwa
wana CCM katika dua zao zote kuhakikisha wanatafuta mgombea waCCM
anayetokana na CCM na siyo yule mgombea aliyepitia CCM na kwamba yeye
mwenyewe anaamini amejitokeza katika wakati sahihi na kwa mahitaji
sahihi yawatanzania na kwamba anaamini akichaguliwa kuwa rais
atawavusha.
Na Suleimna Abeid

0 Comments