Mwakilishi kutoka Ofisi ya Katibu
Mkuu wa Vizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Mushi (wa kwanza kulia)
aliyemwakilishi Dk Donan Mmbando akizungumza na washiriki wa Mkutano
unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za
afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5)
nchini Tanzania. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam kwa siku
mbili mfululizo.
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dk.
Jama Gulaid, akizungumza na washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa
haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na
kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania.
Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo.
Ofisa Mwakilishi Makao Makuu ya Haki za Binadamu duniani, Dk. Jyoti Sanghera.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano
unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za
afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5)
nchini Tanzania. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam kwa siku
mbili mfululizo.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano
unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za
afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5)
nchini Tanzania. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam kwa siku
mbili mfululizo.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano
unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za
afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5)
nchini Tanzania. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam kwa siku
mbili mfululizo.
Ofisa Mwakilishi Kutoka Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini akizungumza na washiriki wa
Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha
huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka
mitano (5) nchini Tanzania. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam
kwa siku mbili mfululizo.
Ofisa Mwakilishi wa Shirika la
Afya Ulimwenguni nchini (WHO), Dk. Rufaro Chatora akizungumza na
washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza
kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini
ya miaka mitano (5) nchini Tanzania. Mkutano huo unafanyika jijini Dar
es Salaam kwa siku mbili mfululizo.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano
unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za
afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5)
nchini Tanzania. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam kwa siku
mbili mfululizo.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano
unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za
afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5)
nchini Tanzania. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam kwa siku
mbili mfululizo.
Ofisa mwakilishi kutoka Umoja wa Mataifa (UN), Dainius Puras akizungumza kwenye mkutano huo.
Mmoja wa waratibu wa mkutano
unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za
afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5)
nchini Tanzania akitoa mwongozo wa majadiliano.
Ofisa Habari wa Kituo cha Taarifa
cha Umoja wa Mataifa (UN), Stella Vuzo akizungumza katika mkutano na
vyombo vya habari vilipozungumza na viongozi wawakilishi walioshiriki
katika mkutano huo.,
Ofisa Mwakilishi Makao Makuu ya
Haki za Binadamu duniani, Dk. Jyoti Sanghera (wa pili kulia) akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa majadiliano.
Wengine ni waofisa mbalimbali walioshiriki mkutano huo wa majadiliano.
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Katibu
Mkuu wa Vizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Mushi (wa kwanza kulia)
aliyemwakilishi Dk Donan Mmbando akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kufungua mkutano wa majadiliano. Akiwa na Maofisa wawakilishi
kutoka taasisi anuai za kimataifa zilizoshiriki majadiliano hayo.
…………………………………………………………………………
Na Joachim Mushi, Dar es Salaam
TANZANIA inajivunia mafanikio
makubwa ya kupunguza idadi ya vifo vya wajawazito pamoja na idadi ya
watoto chini ya miaka mitano wanaopoteza maisha kila mwaka. Mafanikio
hayo yameifanya Tanzania kutolewa mifano kimataifa ikiwa ni kati ya nchi
zilizovuka malengo ya kupunguza idadi hiyo vifo iliyojiwekea kuzifikia.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu
Mkuu wa Vizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando katika
hotuba yake iliyosomwa na mwakilishi wake akifungua mkutano wa
majadiliano na wadau mbalimbali wa utetezi wa haki za binadamu
unaokutana kuangalia namna ya kupunza idadi ya vifo vinavyotokana na
uzazi na vile vya watoto chini ya miaka mitano.
Majadiliano hayo yanayofanyika
jijini Dar es Salaam kwa siku mbili huku yakijikita kuangalia namna
wadau wa haki za binadamu wanavyoweza kuchangia katika kuboresha huduma
za afya na hatimaye kumlinda mtoto chini ya miaka mitano na vifo kwa
ujumla.
Dk. Mmbando alisema Tanzania
imefanikiwa kupunguza vifo vya uzazi na watoto, kutoka idadi ya vifo 166
vilivyokuwa vikitokea kwa kila akinamama 1,000 wanaojifungua mwaka 1990
na kupungua hadi kufikia idadi ya vifo 54 kwa kila akinamama 1,000
mwaka 2012.
Alisema mafanikio hayo ni makubwa
kwani yalivuka malengo iliyokuwa imejiwekea, huku nchi ikitolewa mfano
kati ya mataifa yaliyofanikiwa kiasi kikubwa kupungu vifo vya kesi za
uzazi na huduma za afya kwa ujumla.
Aidha pamoja na hayo alisema bado kuna changamoto mbalimbali za upatikanaji wa huduma za afya kutoka eneo moja hadi lingine, hasa maeneo ya vijijini jambo ambalo Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inakabiliana na changamoto hizo.

Alizishukuru taasisi za Umoja wa
Mataifa (UN) kwa msaada zinazoutoa kupitia taasisi zake mbalimbali
kuisaidia Serikali ya Tanzania kuboresha huduma za afya katika nyanja
tofauti, jambo ambalo ndio chachu ya mafanikio zaidi.
Awali akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dk. Jama Gulaid, aliipongeza Tanzania kwa mafanikio makubwa iliyoyapata katika kupunguza vifo vya uzazi pamoja na watoto chini ya miaka mitano na pia kuwalinda watoto katika kupata huduma bora za afya.

Aliongeza kuwa mafanikio hayo
yanatokana na uongozi mzuri wa Serikali pamoja na nia thabiti ya
viongozi kutambua tatizo na utayari wa kulisimamia kuhakikisha linapata
ufumbuzi, lakini pia usalama wa raia na shughuli zao.
“…Napenda nitumie nafasi hii
kuwasilisha shukrani na dhati kutoka UNICEF kwa Wananchi wote wa
Tanzania kwa kuendelea kulinda haki za watoto, nawapongeza kinamama,
nawapongeza kinababa na viongozi kwa ujumla kwa kulilinda hili…kimsingi
tunaitaji mchango wenu kufanikiwa zaidi,” alisema Dk. Gulaid
akiwahutubia washiriki wa mkutano huo.
Mkutano huo wa siku mbili
unashirikisha wajumbe na wawakilishi kutoka taasisi za kimataifa na
kitaifa zinazoshughulikia masuala ya haki za binadamu, afya na watoto
umeandaliwa na Tume ya Kimataifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa
kushirikiana na Taasisi za Umoja wa Mataifa.
*Imeandaliwa na Mtandao wa www.thehabari.com
*Imeandaliwa na Mtandao wa www.thehabari.com
0 Comments