Advertisement

Responsive Advertisement

IDARA YA UHAMIAJI YAINGIZA SH.BILIONI 474 AWAMU YA NNE YA RAIS JAKAYA KIKWETE


 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii. 
IDARA ya Uhamiaji katika awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete imeingiza zaidi ya Sh.bilioni 474 kwa kipindi cha miaka 10 ambayo imetokana na maboresho mbalimbali katika idara hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamishina wa Fedha na Utawala,Piniel Mgonja amesema kuwa katika awamu ya nne uhamiaji imeweza kufanya kazi ya kisasa kutokana na mifumo pamoja na ujenzi wa Chuocha kuendeleza maafisa wa idara hiyo.

Amesema katika utoaji wa hati ya kusafiria kwa mwezi wanatoa hati 5000 tofauti na miaka 10 iliyopita ambapo walikuwa wakitoa hati 2500 ambayo ilikuwa ikitokana na kuchukua muda mrefu wa kuchapa kuliko ivyo sasa zinachapwa kwa kompyuta.

Mgonja amesema katika suala la uhamiaji bado changamoto kutokana na kuwa na uwazi katika mipaka ambapo walifanya uparesheni kuwakamata zaidi ya watu 74 000 kati ya hao watu zaidi 66000 waliondolewa nchini.
Amesema wamezidi kuimarisha katika udhibiti wa njia za mipaka ili nchi isiweze kugubikwa na wahamiaji haramu.

Amesema katika kipindi kijacho hati kusafiria kwa nchi za Afrika Mashariki itakuwa moja ya kimataifa ili kuondoa usumbufu kwa wateja wao kutafuta mara kwa mara kwa hati ya kusafiria kwa Afrika Mashariki
Kamishina wa Fedha na Utawala wa Idara ya Uhamiaji, Piniel Mgonja akizungumza na waandishi habari juu ya mafanikio ya idara ya uhamiaji katika awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete iliyofanyika leo Makao Makuu ya Idara hiyo Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Makamishina wa Idara ya Uhamiaji wa kwanza kushoto  kutoka mwanzo ,Msemaji wa Idara ya Uhamiaji,Naibu Kamishina wa Idara ya Uhamiaji ,Abbas Irovya ,Naibu Kamishina Mussa Lyamba,Mratibu Mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji ,Petro Malima ,Mhasibu Mkuu Karunde ,pamoja na Mkaguzi wa Idara hiyo, Kyando wakimsikiliza Kamishina wa Fedha na Utawala ,Piniel Mgonja katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini,jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watenadaji wa ngazi za juu wa Idara ya Uhamiaji  pamoja na waandishi wakimsikiliza Kamishina wa Fedha na Utawala wa Idara ya Uhamiaji,Piniel Mgonja katika mkutano  uliofanyika jijini Dar es Salaam.Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Post a Comment

0 Comments