Kikao cha Bunge kilianza kama kawaida
leo July 02 2015, baada ya kipindi cha maswali na majibu yaliyoulizwa
kwa Mawaziri, Mbunge John Mnyika akaomba mwongozo.
“Tumekabidhiwa
orodha ya shughuli za leo.. kimsingi imekiuka kanuni, uamuzi wa kuileta
hii miswada mitatu kwa pamoja kama hati ya dharura umekiuka kabisa
msingi wa makubaliano ya kwenye Semina ambapo Wabunge kwa kauli moja
tulikataa Miswada hii isiletwe kwa hati ya dharura“
Mbunge John Mnyika.
“Naomba Mwongozo, hili jambo linahitaji majibu sasa” >>> Mbunge John Mnyika.
Spika Makinda akaanza kutoa ufafanuzi kuhusu hiyo ishu >>> “Toa kwanza maneno ya kuniamrisha mimi cha kufanya… Hakuna mtu anayeweza kuniamrisha” >>> Anne Makinda.
Spika Anne Makinda.
Spika akaendelea >>> “Tumefanya
mara nyingi sana wala sio leo tu, hakuna kanuni iliyovunjwa na sio mara
ya kwanza kujadili kitu kinachofanana kwa pamoja”>>> Spika Anne Makinda.
Hakukuwa na suluhu ya hilo, Wabunge wa
Upinzani wakagomea Mjadala huo kuendelea ikabidi Kikao cha Bunge
kiahirishwe saa nne asubuhi.
0 Comments