Advertisement

Responsive Advertisement

OFISI YA WAZIRI MKUU YAKAGUA UJENZI WA NYUMBA ZA WAATHIRIKA WA MAAFA YA MVUA YA MAWE NA UPEPO MWAKATA

1
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka (mwenye miwani)  akimsikiliza Mkurugenzi wa  Halmashauri ya  Wilaya ya Msalala, Patrick Karangwa wakati alipokagua  ujenzi  wa nyumba za waathirika wa maafa Kijijini Mwakata, Kahama, tarehe 30 Agosti, 2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
2
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka akimsikiliza mwenyekiti Kijiji cha Mwakata wilayani Kahama, Ezekieli Ramadhani akitafsiri kwa Kiswahili shukrani zizokuwa zikitolewa kwa kisukuma na Bi. Rugumba Msenga kwa serikali kumjengea nyumba  kutokana na  nyumba yake ya awali  kuathirika na maafa ya Mvua, wakati Katibu Mkuu huyo alipokagua ujenzi wa nyumba za waathirika hao zilizojengwa na SUMA JKT, tarehe 30 Agosti, 2015.
3
Muonekano wa nyumba mpya ya muathirika wa maafa ya mvua kijijini Mwakata Kahama. Rugumba Msega (hayupo pichani ) ambayo amejengewa na serikali kupitia Idara ya Uratibu Maafa Ofisi  ya Waziri Mkuu kwa usimamizi wa SUMA JKT, kulia ni makazi ya muda aliyokuwa amejengewa na serikali  na mbele ya nyumba hiyo ni mabaki ya nyumba yake ya awali    iliyoathirika na maafa hayo, tarehe 30 Agosti, 2015.
4
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka akiagana na mwenyekiti Kijiji cha Mwakata wilayani Kahama, Ezekieli Ramadhani mara baada ya kukagua ujenzi wa nyumba za waathirika wa maafa ya mvua  zilizojengwa na SUMA JKT, tarehe 30 Agosti, 2015, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji SUMA JKT,  Kanali Felix Samillan na Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Gen, Mbazi Msuya  (mwenye kofia ).
5
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka (mwenye miwani) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama ( kulia kwake), Benson Mpesya wakiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa shughuli za maafa Mwakata kutoka; Ofisi ya Waziri Mkuu, SUMA JKT, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  Shinyanga, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kahama na Halmashauri ya Msalala  mara baada ya kikao cha  ujenzi wa nyumba za waathirika wa maafa ya mvua  Mwakata, tarehe 30 Agosti, 2015. 

Post a Comment

0 Comments