Advertisement

Responsive Advertisement

Shilole: Nikiiba mume wa mtu nisilaumiwe


Mwanamuziki wa miondoko ya mduara ambaye kwa hivi sasa anatumikia kifungo cha mwaka mmoja kilichotolewa na  Baraza la Sanaa Basata  ya kutojihusisha na shughuli za kisanaa kwa mwaka mmoja  amesema  ameumizwa  mno  na  adhabu  aliyopewa  na  baraza  hilo, hali  inayomfanya  afikirie  kutembea  na  waume  za  watu  ili  aweze  kuyamudu  maisha  yake  ya  kila  siku

Akizungumza na mwandishi wetu, Shilole alisema kuwa adhabu aliyopewa ni kubwa mno kiasi ambacho  anashindwa kuelewa kwa kuwa sanaa ndiyo kazi inayompatia kula na hata kuwasomesha watoto wake hivyo kumfungia mwaka mzima ni kama kumtuma kutembea hata na waume za watu  ili maisha yake yazidi kusonga mbele.

“ Mimi naona sasa wananituma kuanza kusaka waume za watu kwa kweli kwa sababu mwaka mzima kweli na ni kazi ambayo naitegemea kwa kila kitu katika maisha yangu kwa nini  mtu usiwaze vitu vingine kama huna kazi ya kufanya jamani, yaani inaniuma sana,” alisema Shilole.
Mpekuzi blog

Post a Comment

0 Comments