Makada imara wa CCM Field Marshall Mwigulu Nchemba na Dkt. Hamis Kigwangalla waki-Magufulika kuonesha sapoti kwa Mgombea wao Dkt. John Pombe Magufuli aliyefanya tukio hilo siku si nyingi kwenye Jukwaa la Kampeni.
Field Marshall Mwigulu Nchemba akilakiwa kwa nderemo mjini Nzega
Dkt Hamisi Kigwangalla akiwasili kwenye Ufunguzi wa kampeni za Ubunge jimbo la Nzega Mjini.Mjumbe
wa timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi Field Marshall Mwigulu
NChemba ambaye ameanza safari za Anga-kwa-Anga kusaka kura Nchi
nzima,Hapa akizungumza na Wananchi wa Nzega namna CCM ilivyosimamisha
Mgombea Bora wa Urais ambaye sifa yake kuwa ni KAZI TU na rafiki yake
Mkubwa ni TANZANIA. Comrade Mwigulu amesema, Uchaguzi wa mwaka 2015 ni
mwepesi sana kwa CCM kwa kuwa wagombea wote ni zao la Chama tawala na
wanawajua vizuri.
Mbunge
Ubunge wa jimbo la Nzega Mjini Ndg. Hussein Bashe akizungumza na
Wananchi wake wakati wa Ufunguzi wa kampeni kwa Jimbo la Nzega Mjini.
Bashe amewaomba Wana-Nzega kumpatia ridhaa ya kuwa mbunge wa Jimbo hilo
ili aweze kusimamia vyema shughuli za Maendeleo kama Uimarishaji wa
Huduma za Afya kwa Hospitali ya Nzega, Kusimamia haki za Bodaboda na
Mamantilie wa Nzega, shughuli za Halmashauri ya Mji wa Nzega kwa
Ufanisi.Pia amesisitiza yeye ni TEAM MAGUFULI na anaamini Maendeleo ya
kweli na ya kasi yataletwa na Magufuli kwa awamu hii ya tano ya Uongozi
wa Taifa letu.Mbunge
Mtarajiwa wa Chama cha Mapinduzi Jimbo jipya la Nzega Vijijini Dkt.
Hamis Kigwangala akisalimiana na Wananchi wa Nzega mjini alipokwenda
kusapoti Ufunguzi wa kampeni za Mgombea Jirani Ndg.Hussein Bashe. Picha zote na Sanga Festo Jr
Mpekuzi blog
0 Comments