Askofu mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Rev. Josephat Gwajima ametoa Onyo kali kwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM (taifa), bwana Abdallah Bulembo kwa kulitaja jina lake katika mkutano wa kampeni za CCM huko Singida.
Onyo hilo limetolewa jana na Askofu Gwajima mbele ya waumini wake huku akimtahadharisha Bulembo kuwa iwapo ataendelea, basi na yeye ataibuka kutoka mafichoni ili kujibu mashambulizi.
"Nakuonya
Bulembo, uache kunitaja kwenye mikutano yenu ya
kampeni.Ukiendelea kunitaja, nitapanda helkopta nikufuate huko
huko ili nijibu mapigo. Sitakujibu peke yako, ntawajibu na
waliokutuma.
"Nawatuma watu wa CCM mliopo kanisani kwangu mmwambie Bulembo aniache. Nikimjibu atasikitika.
"Nikiwajibu, utatoka moshi na hawatafungua macho. Ntawajibu wote na waliomtuma hadi nchi itatikisika."-Gwajima
Akiwa mkoani Singida kwenye mikutano ya kampeni za mgombea urais wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, Bulembo anadaiwa kumtuhumu Gwajima kwa kuandaa machafuko ili kuharibu amani ya nchi.
Akiwa mkoani Singida kwenye mikutano ya kampeni za mgombea urais wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, Bulembo anadaiwa kumtuhumu Gwajima kwa kuandaa machafuko ili kuharibu amani ya nchi.
Bonyeza hapo chini umsikilize Gwajima.
0 Comments